Friday 13 August 2010

Mapishi ya Ugali na dagaa



Mahitaji

  • Dagaa (dried anchovies packet 1)
  • Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
  • Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2)
  • Kitunguu maji (onion 1)
  • Limao (lemon 1/4)
  • Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
  • Chumvi (salt 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil) 
  • Hoho (green pepper)
Matayarisho

Chambua dagaa kwa kutoa vichwa vyao na utumbo, baada ya hapo waloeke katkika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 na uaoshe tena katika maji ya baridi na uwakaushe uwaweke pembeni. Ukishamaliza katakata kitunguu na uandae nyanya tayari kwa upishi. Bandika sufuria ya kupikia dagaa jikoni na utie mafuta, yakishapata moto tia vitunguu pamoja na dagaa. Kaanga mpaka dagaa wawe light brown kisha tia nyanya, chumvi na pilipili. Pika nyanya mpaka ziive (ukitaka kujua kama nyanya zimeiva utaona zinatengana na mafuta) Baada ya hapo kamulia limao kidogo sana na tia pilipili hoho na zipike kama dakika mbili. kisha ipua.
Ukisha maliza kupika dagaa andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.

1 comment:

  1. asante mamaa kwa upendo na muda unaotumia kutuelimisha mi niko america si unajua tena vyakula vya huku all I want to say tunashukuru sana mungu akuweke mamaa ongera sana kwa mtoto tunaomba ukiandika utupe vipimo vya ml au cups asante sana mamaa god bless

    ReplyDelete